Usambazaji chakula ni dhana ya ubebaji chakula kutoka kwa mpishi au mghahawa kwenda kwa mlaji. Dhana hii imekuwepo kwa muda nchini Tanzania ikizingatiwa kwamba asilimia 60% ya akina mama nchini Tanzania hujishughulisha na biashara ya chakula. Read more
Usambazaji chakula ni dhana ya ubebaji chakula kutoka kwa mpishi au mghahawa kwenda kwa mlaji. Dhana hii imekuwepo kwa muda nchini Tanzania ikizingatiwa kwamba asilimia 60% ya akina mama nchini Tanzania hujishughulisha na biashara ya chakula.
Mbali na kwamba utawaona wasaidizi wengi wa mama lishe wakitafuta na kusambaza chakula, mfumo huu pia wa usambazaji wa chakula umekuwa ukifanywa na baadhi ya migahawa japokuwa si rasmi.
Kimaksudi, nitaangazia mfumo ambao umekuwa ukitumiwa Biashara ya huduma za usambazaji wa chakula zinaongezeka katika miji mikubwa. Wafanyabishara ya chakula walikuwa wakichapisha menyu pamoja bei zake, (huku chini ya menyu hizo wakiwa wameweka namba zao za simu) na kuzisambaza maofisini tayari wanangoja kupigiwa simu na kupewa oda. Njia hii umlazimu mteja kupiga simu na kuuliza ikiwa chakula hiki au kile kipo ama hakipo… kisha ukubaliana na muuzaji na hivyo chakula ufungwa na kupelekewa kwa mteja.
Mbinu hii inatumika hata sasa kwa baadhi ya migahawa!
Changamoto kuu ambazo watumiaji wa mfumo huu wanakabiliana nazo ni, kwanza, umlazimu mteja kupiga simu kuweka oda na kufuatilia maendeleo ya oda. Pili, restaurant ni moja na hivyo inamlazimu mteja ale chakula kilichopo na si kile anapenda kula. Tatu, kukosekana kwa mfumo thabiti wa usambazaji chakula, n.k.
Hai Ilivyo Sasa!
Makuzi na ongezeko la matumizi ya technolojia duniani yamebadili namna biashara nyingi zinavyofanyika. Usambazaji chakula nao hujaachwa nyuma. Japo kwa Tanzania teknolojia bado haijashika kasi lakini mambo yameanza yanabadilika. Japo hatuna takwimu rasmi, lakini inasemekana zaidi ya oda 2000 uwekwa kupitia smartphone na kusambazwa kwa wateja jijini Dar es Salaam kila siku.
Kupitia applications za simu, watumiaji wa Android na iPhone wanaweza kuagiza chakula kupitia aidha Agiza24, Piki, Yamee, FoodSasa, n.k na wakafikishiwa mahali walipo katika mikoa yao.
Wateja ndiyo huwajibika kulipa gharama ya usafiri, vifungashio na n.k. Hivyo, wateja wa huduma hizi ni wale wenye uwezo wa kulipia gharama hizi za ziada. Kumbe kwa kadri nchi inavyokuwa na idadi ndogo ya raia wenye kipato cha kati na kwenda juu, ndivyo idadi ya watumiaji wa huduma hizi inavyoendelea kuwa ndogo.
Hata hivyo inatarajiwa kwamba, ukuaji wa matumizi ya teknologia kama inavyoshuhudiwa sasa, kidogo kidogo itabadili tabia na mienendo ya watu katika shughuli za kila siku. Kwa msingi huo inatarajiwa miaka mitano kuanzia sasa idadi ya watumiaji wa huduma hizi itaongezeka maradufu.
Read less