Hapo chini ni picha ya madereva 42 wa FoodPanda wakiwa nje ya nyumba ya amayoishi msichana wa miaka 17 na oda yake, huko Ufilipino. Msichana alikuwa nyumbani yeye na bibi yake na akapata wazo la kuagiza chakula kupitia program wezeshi ...Read more
Hapo chini ni picha ya madereva 42 wa FoodPanda wakiwa nje ya nyumba ya amayoishi msichana wa miaka 17 na oda yake, huko Ufilipino.
Msichana alikuwa nyumbani yeye na bibi yake na akapata wazo la kuagiza chakula kupitia program wezeshi ya simu, yaani mobile application. Aliingia kwenye Application ya FoodPanda na akatafuta na kuagiza chips kuku mbili kwa ajili yake na bibi yake. Kwa sababu ya aidha mtandao wa intaneti ulikuwa wa polepole au shida za programu wezeshi (yaani application) hakuweza kukamilisha oda na alibofya kitufe cha ‘weka oda’ zaidi ya mara 40 na hakikufanya kazi. Mwishowe, app ilifanya kazi na oda yake ikafanikiwa kuwekwa. Pasina kujuwa kuwa kila wakati alipofya kitufe cha ‘weka oda’ ili kukamilisha oda, oda ilitumwa na hivyo kufanikiwa kuwekwa 😂
Baada ya muda, walikuja madereva wasambazi 42 nje ya nyumba yake, idadi sawa kutoka kwa mgahawa ule ule. 😒 !!
Lakini binti huyo alikuwa na pesa za kulipia oda moja tu hiyo… alikuwa na pesa 189, sawa na dola 5 hivi au zaidi.
Jumla ya oda 42 ilikuwa ni zaidi ya pesa 5000 na hivyo hasingeweza kulipa zote. Lakini majirani wote wa nyumba ile walikuja na kununua chakula kilichobaki ili kumsaidia kulipa gharama!!
Lakini unajua nini?!! Najua watu wengine ambao wangeweza kulipia oda hizo zote na kula 🤣🤣